Native Bible

Daniel 1:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Baadaye ulinganishe sura zetu na vijana wanaokula chakula cha mfalme, ukawatendee watumishi wako kulingana na unachoona.”

Daniel 1:13 in English

Daniel 1:13 · Berean Standard Bible

Then compare our appearances with those of the young men who are eating the royal food, and deal with your servants according to what you see.”

Context

11Ndipo Danieli akamwambia mlinzi aliyeteuliwa na huyo mkuu wa maafisa kuwasimamia Danieli, Hanania, Mishaeli na Azaria, 12“Tafadhali wajaribu watumishi wako kwa siku kumi. Usitupe chochote ila nafaka na mboga za majani* tule, na maji ya kunywa. 13Baadaye ulinganishe sura zetu na vijana wanaokula chakula cha mfalme, ukawatendee watumishi wako kulingana na unachoona.” 14Basi akakubali jambo hili, akawajaribu kwa siku kumi. 15Mwisho wa zile siku kumi, walionekana kuwa na afya na kunawiri zaidi kuliko yeyote kati ya wale vijana waliokula chakula cha mfalme.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.