Wakolosai 2:3
Colossians 2:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
ambaye ndani yake kumefichwa hazina zote za hekima na maarifa.
Colossians 2:3 in English
Colossians 2:3 · Berean Standard Bible
in whom are hidden all the treasures of wisdom and knowledge.
Context
1Nataka mjue jinsi ninavyojitaabisha kwa ajili yenu na kwa ajili ya wale walioko Laodikia, na pia kwa ajili ya wote ambao hawajapata kuniona mimi binafsi. 2Kusudi langu ni watiwe moyo na kuunganishwa katika upendo, ili wapate ule utajiri wa ufahamu mkamilifu, ili waijue siri ya Mungu, yaani, Kristo mwenyewe, 3ambaye ndani yake kumefichwa hazina zote za hekima na maarifa. 4Nawaambia mambo haya ili mtu yeyote asiwadanganye kwa maneno ya kuwashawishi. 5Kwa kuwa ingawa mimi siko pamoja nanyi kimwili, lakini niko pamoja nanyi kiroho, nami nafurahi kuuona utaratibu wenu na jinsi uthabiti wa imani yenu katika Kristo ulivyo.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.