Amosi 9:2
Amos 9:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wajapojichimbia chini mpaka kwenye vina vya kuzimu, kutoka huko mkono wangu utawatoa. Wajapopanda juu hadi kwenye mbingu, kutoka huko nitawashusha.
Amos 9:2 in English
Amos 9:2 · Berean Standard Bible
Though they dig down to Sheol, from there My hand will take them; and though they climb up to heaven, from there I will pull them down.
Context
1Nilimwona Bwana akiwa amesimama kando ya madhabahu, naye akasema:
“Piga vichwa vya nguzo
ili vizingiti vitikisike.
Viangushe juu ya vichwa vya watu wote;
na wale watakaosalia nitawaua kwa upanga.
Hakuna awaye yote atakayekimbia,
hakuna atakayetoroka. 2Wajapojichimbia chini mpaka kwenye vina vya kuzimu,
kutoka huko mkono wangu utawatoa.
Wajapopanda juu hadi kwenye mbingu,
kutoka huko nitawashusha. 3Wajapojificha juu ya kilele cha Karmeli,
huko nitawawinda na kuwakamata.
Wajapojificha kutoka kwenye uso wangu
katika vilindi vya bahari,
huko nako nitaamuru joka kuwauma. 4Wajapopelekwa uhamishoni na adui zao,
huko nako nitaamuru upanga uwaue.
Nitawakazia macho yangu kwa mabaya
wala si kwa mazuri.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.