Amosi 7:10
Amos 7:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kisha Amazia kuhani wa Betheli akatuma ujumbe kwa Yeroboamu mfalme wa Israeli, akisema: “Amosi analeta fitina juu yako katikati ya Israeli. Nchi haiwezi kuvumilia maneno yake yote.
Amos 7:10 in English
Amos 7:10 · Berean Standard Bible
Then Amaziah the priest of Bethel sent word to Jeroboam king of Israel, saying, “Amos has conspired against you in the midst of the house of Israel. The land cannot bear all his words,
Context
8Naye Bwana akaniuliza, “Je, Amosi unaona nini?”
Nikamjibu, “Uzi wa timazi.”
Kisha Bwana akasema, “Tazama, ninaweka uzi wa timazi miongoni mwa watu wangu Israeli; sitawahurumia tena. 9“Mahali pa Isaki pa juu pa kuabudia miungu pataangamizwa,
na mahali patakatifu pa Israeli pa kuabudia pataharibiwa;
kwa upanga wangu nitainuka
dhidi ya nyumba ya Yeroboamu.” 10Kisha Amazia kuhani wa Betheli akatuma ujumbe kwa Yeroboamu mfalme wa Israeli, akisema: “Amosi analeta fitina juu yako katikati ya Israeli. Nchi haiwezi kuvumilia maneno yake yote. 11Kwa kuwa hili ndilo Amosi analosema:
“ ‘Yeroboamu atakufa kwa upanga,
na kwa hakika Israeli watakwenda uhamishoni,
mbali na nchi yao.’ ” 12Kisha Amazia akamwambia Amosi, “Nenda zako, ewe mwonaji! Urudi katika nchi ya Yuda. Ujipatie riziki yako huko na kutoa unabii wako.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.