Amosi 4:2
Amos 4:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Bwana Mwenyezi ameapa kwa utakatifu wake: “Hakika wakati utakuja mtakapochukuliwa na kulabu, na wanaosalia kwa ndoana za samaki.
Amos 4:2 in English
Amos 4:2 · Berean Standard Bible
The Lord GOD has sworn by His holiness: “Behold, the days are coming when you will be taken away with hooks, and your posterity with fishhooks.
Context
1Sikilizeni neno hili, ninyi ngʼombe wa Bashani
mlioko juu ya Mlima Samaria,
ninyi wanawake mnaowaonea maskini,
na kuwagandamiza wahitaji,
na kuwaambia wanaume wenu,
“Tuleteeni vinywaji!” 2Bwana Mwenyezi ameapa kwa utakatifu wake:
“Hakika wakati utakuja
mtakapochukuliwa na kulabu,
na wanaosalia kwa ndoana za samaki. 3Nanyi mtakwenda moja kwa moja
kupitia mahali palipobomolewa kwenye ukuta,
nanyi mtatupwa nje kuelekea Harmoni,”
asema Bwana. 4“Nendeni Betheli mkatende dhambi;
nendeni Gilgali mkazidi kutenda dhambi.
Leteni dhabihu zenu kila asubuhi,
zaka zenu kila mwaka wa tatu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.