Amosi 4:11
Amos 4:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Niliwaangamiza baadhi yenu kama nilivyoangamiza Sodoma na Gomora. Mlikuwa kama kijiti kiwakacho kilichonyakuliwa motoni, hata hivyo hamjanirudia,” asema Bwana.
Amos 4:11 in English
Amos 4:11 · Berean Standard Bible
“Some of you I overthrew as I overthrew Sodom and Gomorrah, and you were like a firebrand * snatched from a blaze, yet you did not return to Me,” declares the LORD.
Context
9“Mara nyingi nilizipiga bustani zenu na mashamba ya mizabibu,
niliyapiga kwa kutu na ukungu.
Nzige walitafuna tini zenu na miti ya mizeituni,
hata hivyo hamjanirudia mimi,”
asema Bwana. 10“Niliwapelekea tauni miongoni mwenu
kama nilivyofanya kule Misri.
Niliwaua vijana wenu wa kiume kwa upanga,
niliwachukua farasi wenu.
Nilijaza pua zenu kwa uvundo kutoka kwenye kambi zenu,
hata hivyo hamjanirudia mimi,”
asema Bwana. 11“Niliwaangamiza baadhi yenu kama
nilivyoangamiza Sodoma na Gomora.
Mlikuwa kama kijiti kiwakacho kilichonyakuliwa motoni,
hata hivyo hamjanirudia,”
asema Bwana. 12“Kwa hiyo hili ndilo nitakalowafanyia, Israeli,
na kwa sababu nitawafanyia hili,
jiandaeni kukutana na Mungu wenu, ee Israeli.” 13Yeye ambaye hufanya milima, anaumba upepo,
na kufunua mawazo yake kwa mwanadamu,
yeye ageuzaye asubuhi kuwa giza,
na kukanyaga mahali pa juu pa nchi:
Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.