Amosi 3:8
Amos 3:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Simba amenguruma: je, ni nani ambaye hataogopa? Bwana Mwenyezi ametamka: je, ni nani awezaye kukosa kutoa unabii?
Amos 3:8 in English
Amos 3:8 · Berean Standard Bible
The lion has roared— who will not fear? The Lord GOD has spoken— who will not prophesy?
Context
6Je, tarumbeta inapopigwa mjini kujulisha hatari,
watu hawatetemeki?
Mji upatwapo na maafa,
je, si Bwana amesababisha? 7Hakika Bwana Mwenyezi hatafanya neno lolote
bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake. 8Simba amenguruma:
je, ni nani ambaye hataogopa?
Bwana Mwenyezi ametamka:
je, ni nani awezaye kukosa kutoa unabii? 9Tangazeni katika ngome za Ashdodi
na katika ngome za Misri:
“Kusanyikeni juu ya milima ya Samaria;
angalieni wingi wa wasiwasi ulio ndani yake,
na uonevu ulio miongoni mwa watu wake.” 10Bwana asema: “Hawajui kutenda lililo jema,
wale ambao hujilundikia nyara
na vitu vilivyotekwa katika ngome zao.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.