Matendo 8:15
Acts 8:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nao walipofika wakawaombea ili wampokee Roho Mtakatifu,
Acts 8:15 in English
Acts 8:15 · Berean Standard Bible
On their arrival, they prayed for them to receive the Holy Spirit.
Context
13Simoni naye akaamini na akabatizwa. Akamfuata Filipo kila mahali, akistaajabishwa na ishara kuu na miujiza aliyoiona. 14Basi mitume waliokuwa Yerusalemu waliposikia kuwa Samaria wamelipokea neno la Mungu, wakawatuma Petro na Yohana waende huko. 15Nao walipofika wakawaombea ili wampokee Roho Mtakatifu, 16kwa sababu Roho Mtakatifu alikuwa bado hajawashukia hata mmoja ila wamebatizwa tu katika jina la Bwana Yesu. 17Ndipo Petro na Yohana wakaweka mikono yao juu ya wale waliobatizwa, nao wakapokea Roho Mtakatifu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.