Native Bible

Acts 6:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Wakawachochea watu, wazee na walimu wa Sheria, nao wakamkamata Stefano wakamfikisha mbele ya baraza.

Acts 6:12 in English

Acts 6:12 · Berean Standard Bible

So they stirred up the people, elders, and scribes and confronted Stephen. They seized him and brought him before the Sanhedrin,*

Context

10Lakini hawakuweza kushindana na hekima yake wala huyo Roho ambaye alisema kwake. 11Ndipo kwa siri wakawashawishi watu fulani waseme, “Tumemsikia Stefano akisema maneno ya kufuru dhidi ya Mose na dhidi ya Mungu.” 12Wakawachochea watu, wazee na walimu wa Sheria, nao wakamkamata Stefano wakamfikisha mbele ya baraza. 13Wakaweka mashahidi wa uongo ambao walishuhudia wakisema, “Mtu huyu kamwe haachi kusema dhidi ya mahali hapa patakatifu na dhidi ya Sheria. 14Kwa maana tumemsikia akisema kwamba Yesu wa Nazareti atapaharibu mahali patakatifu na kubadili desturi zote tulizopewa na Mose.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.