Matendo 5:22
Acts 5:22 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini wale walinzi wa Hekalu walipokwenda gerezani hawakuwakuta mitume mle. Kwa hiyo wakarudi na kutoa habari.
Acts 5:22 in English
Acts 5:22 · Berean Standard Bible
But on arriving at the jail, the officers did not find them there. So they returned with the report:
Context
20“Nendeni, mkasimame Hekaluni mkawaambie watu maneno yote ya uzima huu mpya.” 21Waliposikia haya wakaenda Hekaluni alfajiri wakaendelea kufundisha watu.
Kuhani mkuu na wale waliokuwa pamoja nao walipowasili, alikusanya baraza na wazee wote wa Israeli wakatuma wale mitume waletwe kutoka gerezani. 22Lakini wale walinzi wa Hekalu walipokwenda gerezani hawakuwakuta mitume mle. Kwa hiyo wakarudi na kutoa habari. 23Wakasema, “Tumekuta milango ya gereza imefungwa sawasawa na askari wa gereza wamesimama nje ya mlango, lakini tulipofungua milango hakuwepo mtu yeyote ndani.” 24Basi mkuu wa walinzi wa Hekalu na viongozi wa makuhani waliposikia haya, wakafadhaika na kushangaa sana kwa ajili yao kwamba jambo hili litakuwaje.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.