Matendo 3:20
Acts 3:20 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
naye apate kumtuma Kristo, ambaye ameteuliwa kwa ajili yenu, yaani Yesu.
Acts 3:20 in English
Acts 3:20 · Berean Standard Bible
that times of refreshing may come from the presence of the Lord, and that He may send Jesus, the Christ, who has been appointed for you.
Context
18Lakini kwa njia hii Mungu alitimiza kile ambacho alikuwa ametabiri kwa vinywa vya manabii wake wote, kwamba Kristo* atateswa. 19Tubuni basi mkamgeukie Mungu, dhambi zenu zifutwe, ili zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwepo kwake Bwana, 20naye apate kumtuma Kristo, ambaye ameteuliwa kwa ajili yenu, yaani Yesu. 21Ilimpasa mbingu zimpokee mpaka wakati wa kufanywa upya kila kitu, kama Mungu alivyoahidi zamani kupitia kwa vinywa vya manabii wake watakatifu. 22Kwa maana Mose alisema, ‘Bwana Mungu wenu atawainulia nabii kama mimi kutoka miongoni mwa ndugu zenu. Itawapasa kumtii huyo kwa kila jambo atakalowaambia.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.