Matendo 27:38
Acts 27:38 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Baada ya watu wote kula chakula cha kutosha, wakapunguza uzito wa meli kwa kutupa ngano baharini.
Acts 27:38 in English
Acts 27:38 · Berean Standard Bible
After the men had eaten their fill, they lightened the ship by throwing the grain into the sea.
Context
36Ndipo wote wakatiwa moyo, wakaanza kula chakula. 37Ndani ya meli tulikuwa jumla ya watu 276. 38Baada ya watu wote kula chakula cha kutosha, wakapunguza uzito wa meli kwa kutupa ngano baharini. 39Kulipopambazuka, mabaharia hawakuitambua ile nchi, lakini waliona ghuba yenye ufuko wa mchanga, ambako waliamua kuipweleza meli kama ingewezekana. 40Kwa hiyo wakatupa nanga zote na kuziacha baharini, na wakati huo huo wakalegeza kamba zilizokuwa zikishikilia usukani wa meli. Kisha wakatweka tanga la mbele lishike upepo na kuisukuma meli kuelekea pwani.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.