Matendo 27:36
Acts 27:36 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ndipo wote wakatiwa moyo, wakaanza kula chakula.
Acts 27:36 in English
Acts 27:36 · Berean Standard Bible
They were all encouraged and took some food themselves.
Context
34Kwa hiyo nawasihi mle chakula, kwa maana itawasaidia ili mweze kuishi. Kwa kuwa hakuna hata mmoja wenu atakayepoteza unywele hata mmoja kutoka kichwani mwake.” 35Baada ya kusema maneno haya, Paulo akachukua mkate, akamshukuru Mungu mbele yao wote, akaumega akaanza kula. 36Ndipo wote wakatiwa moyo, wakaanza kula chakula. 37Ndani ya meli tulikuwa jumla ya watu 276. 38Baada ya watu wote kula chakula cha kutosha, wakapunguza uzito wa meli kwa kutupa ngano baharini.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.