Matendo 27:29
Acts 27:29 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wakiogopa kwamba meli yetu ingegonga kwenye miamba, wakashusha nanga nne za nyuma ya meli, wakawa wanaomba kupambazuke.
Acts 27:29 in English
Acts 27:29 · Berean Standard Bible
Fearing that we would run aground on the rocks, they dropped four anchors from the stern and prayed for daybreak.
Context
27Usiku wa kumi na nne ulipofika, tulikuwa bado tunasukumwa na upepo katika Bahari ya Adria. Ilipokuwa yapata usiku wa manane, mabaharia wakahisi kwamba walikuwa wanakaribia nchi kavu. 28Kwa hiyo wakapima kina cha maji na kukuta kilikuwa pima ishirini,* baada ya kuendelea mbele kidogo wakapima tena wakapata kina cha pima kumi na tano.* 29Wakiogopa kwamba meli yetu ingegonga kwenye miamba, wakashusha nanga nne za nyuma ya meli, wakawa wanaomba kupambazuke. 30Katika jaribio la kutoroka kutoka kwenye meli, mabaharia wakashusha mashua ya kuokolea watu baharini, wakijifanya kwamba wanakwenda kushusha nanga za omo.* 31Ndipo Paulo akamwambia yule jemadari na askari, “Hawa watu wasipobaki katika meli, hamtaweza kuokoka.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.