Matendo 22:9
Acts 22:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Basi wale watu waliokuwa pamoja nami waliiona ile nuru, lakini hawakuisikia sauti ya yule aliyekuwa akisema nami.
Acts 22:9 in English
Acts 22:9 · Berean Standard Bible
My companions saw the light, but they could not understand the voice of the One speaking to me.
Context
7Nikaanguka chini, nikasikia sauti ikiniambia, ‘Sauli, Sauli! Mbona unanitesa?’ 8“Nikajibu, ‘Wewe ni nani Bwana?’
“Naye akaniambia, ‘Mimi ni Yesu wa Nazareti unayemtesa.’ 9Basi wale watu waliokuwa pamoja nami waliiona ile nuru, lakini hawakuisikia sauti ya yule aliyekuwa akisema nami. 10“Nikauliza, ‘Nifanye nini Bwana?’
“Naye Bwana akaniambia, ‘Inuka uingie Dameski, huko utaambiwa yote yakupasayo kufanya.’ 11Kwa kuwa nilikuwa siwezi kuona kwa ajili ya mngʼao wa ile nuru, wenzangu wakanishika mkono wakaniongoza kuingia Dameski.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.