Native Bible

Acts 21:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Siku iliyofuata tukaondoka, tukafika Kaisaria. Huko tukaenda nyumbani kwa mwinjilisti mmoja jina lake Filipo, aliyekuwa mmoja wa wale Saba, tukakaa kwake.

Acts 21:8 in English

Acts 21:8 · Berean Standard Bible

Leaving the next day, we went on to Caesarea and stayed at the home of Philip the evangelist, who was one of the Seven.*

Context

6Baada ya kuagana, tukapanda melini, nao wakarudi majumbani mwao. 7Tukaendelea na safari yetu toka Tiro tukafika Tolemai, tukawasalimu ndugu wa huko, tukakaa nao kwa siku moja. 8Siku iliyofuata tukaondoka, tukafika Kaisaria. Huko tukaenda nyumbani kwa mwinjilisti mmoja jina lake Filipo, aliyekuwa mmoja wa wale Saba, tukakaa kwake. 9Filipo alikuwa na binti wanne mabikira waliokuwa wanatoa unabii. 10Baada ya kukaa kwa siku kadhaa, akateremka nabii mmoja kutoka Uyahudi jina lake Agabo.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.