Matendo 21:22
Acts 21:22 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Sasa tufanyeje? Bila shaka watasikia kwamba umekuja Yerusalemu.
Acts 21:22 in English
Acts 21:22 · Berean Standard Bible
What then should we do? They will certainly hear that you have come.
Context
20Baada ya kusikia mambo haya wakamwadhimisha Mungu. Ndipo wakamwambia Paulo, “Ndugu, unaona kulivyo na maelfu ya Wayahudi walioamini, nao wote wana juhudi kwa ajili ya sheria. 21Lakini wameambiwa habari zako kwamba unafundisha Wayahudi wote waishio miongoni mwa watu wa Mataifa kumkataa Mose, na kwamba unawaambia wasiwatahiri watoto wao wala kufuata desturi zetu. 22Sasa tufanyeje? Bila shaka watasikia kwamba umekuja Yerusalemu. 23Kwa hiyo fanya lile tunalokuambia. Tunao watu wanne hapa ambao wameweka nadhiri. 24Jiunge na watu hawa, mfanye utaratibu wa ibada ya kujitakasa pamoja nao, na ulipe gharama ili wanyoe nywele zao. Kwa njia hii kila mtu atafahamu ya kuwa mambo waliyosikia si ya kweli na kwamba wewe unaishika sheria.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.