Native Bible

Acts 2:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Zikatokea ndimi kama za moto zilizogawanyika na kukaa juu ya kila mmoja wao.

Acts 2:3 in English

Acts 2:3 · Berean Standard Bible

They saw tongues like flames of fire that separated and came to rest on each of them.

Context

1Siku ya Pentekoste ilipowadia, waamini wote walikuwa mahali pamoja. 2Ghafula sauti kama mvumo mkubwa wa upepo mkali uliotoka mbinguni ukaijaza nyumba yote walimokuwa wameketi. 3Zikatokea ndimi kama za moto zilizogawanyika na kukaa juu ya kila mmoja wao. 4Wote wakajazwa na Roho Mtakatifu, wakaanza kunena kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia. 5Basi walikuwepo Yerusalemu Wayahudi wanaomcha Mungu kutoka kila taifa chini ya mbingu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.