Native Bible

Acts 11:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Ndipo nikasikia sauti ikiniambia, ‘Petro, ondoka uchinje na ule.’

Acts 11:7 in English

Acts 11:7 · Berean Standard Bible

Then I heard a voice saying to me, ‘Get up, Peter, kill and eat.’

Context

5“Nilikuwa katika mji wa Yafa nikiomba, nami nikapitiwa na usingizi wa ghafula, nikaona maono. Kulikuwa na kitu kama nguo kubwa ikishuka kutoka mbinguni, ikishushwa kwa ncha zake nne, nayo ikanikaribia. 6Nilipoangalia ndani yake kwa karibu niliona wanyama wenye miguu minne wa nchini, wanyama wa mwitu, watambaao na ndege wa angani. 7Ndipo nikasikia sauti ikiniambia, ‘Petro, ondoka uchinje na ule.’ 8“Nikajibu, ‘La hasha Bwana! Kitu chochote kilicho najisi hakijaingia kinywani mwangu.’ 9“Sauti ikasema kutoka mbinguni mara ya pili, ‘Usikiite najisi kitu chochote Mungu alichokitakasa.’

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.