Native Bible

Acts 11:27 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Wakati huo manabii walishuka toka Yerusalemu hadi Antiokia.

Acts 11:27 in English

Acts 11:27 · Berean Standard Bible

In those days some prophets came down from Jerusalem to Antioch.

Context

25Kisha Barnaba akaenda Tarso kumtafuta Sauli, 26naye alipompata akamleta Antiokia. Hivyo kwa mwaka mzima Barnaba na Sauli wakakutana na kanisa na kufundisha idadi kubwa ya watu. Ilikuwa ni katika kanisa la Antiokia kwa mara ya kwanza wanafunzi waliitwa Wakristo. 27Wakati huo manabii walishuka toka Yerusalemu hadi Antiokia. 28Mmoja wao, jina lake Agabo, akasimama akatabiri kwa uweza wa Roho Mtakatifu kwamba njaa kubwa itaenea ulimwengu mzima. Njaa hiyo ilitokea wakati wa utawala wa Klaudio. 29Mitume wakaamua kwamba kila mtu, kulingana na uwezo alio nao, atoe msaada kwa ajili ya ndugu wanaoishi Uyahudi.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.