Matendo 10:8
Acts 10:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Akawaambia mambo yote yaliyotukia, kisha akawatuma waende Yafa.
Acts 10:8 in English
Acts 10:8 · Berean Standard Bible
He explained what had happened and sent them to Joppa.
Context
6Yeye anaishi na Simoni mtengenezaji ngozi ambaye nyumba yake iko kando ya bahari.” 7Yule malaika aliyekuwa akizungumza naye alipoondoka, Kornelio akawaita watumishi wake wawili pamoja na askari mmoja mcha Mungu aliyekuwa miongoni mwa wale waliomtumikia. 8Akawaambia mambo yote yaliyotukia, kisha akawatuma waende Yafa. 9Siku ya pili yake, walipokuwa wameukaribia mji, wakati wa adhuhuri, Petro alipanda juu ya nyumba kuomba. 10Alipokuwa akiomba akahisi njaa, akatamani kupata chakula. Lakini wakati walikuwa wakiandaa chakula, akalala usingizi mzito sana.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.