Matendo 10:20
Acts 10:20 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Inuka na ushuke, usisite kwenda nao kwa kuwa mimi nimewatuma.”
Acts 10:20 in English
Acts 10:20 · Berean Standard Bible
So get up! Go downstairs and accompany them without hesitation, because I have sent them.”
Context
18Wakabisha hodi na kuuliza kama Simoni aliyeitwa Petro alikuwa anaishi hapo. 19Wakati Petro akiwa anafikiria juu ya yale maono, Roho Mtakatifu akamwambia, “Simoni, wako watu watatu wanaokutafuta. 20Inuka na ushuke, usisite kwenda nao kwa kuwa mimi nimewatuma.” 21Petro akashuka na kuwaambia wale watu waliokuwa wametumwa kutoka kwa Kornelio, “Mimi ndiye mnayenitafuta. Mmekuja kwa sababu gani?” 22Wale watu wakamjibu, “Tumetumwa na Kornelio yule jemadari. Yeye ni mtu mwema anayemcha Mungu, na anaheshimiwa na Wayahudi wote. Yeye ameagizwa na malaika mtakatifu akukaribishe nyumbani kwake, ili asikilize maneno utakayomwambia.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.