2 Timotheo 3:13
2 Timothy 3:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini watu waovu na wadanganyaji watazidi kuwa waovu, wakidanganya na kudanganyika.
2 Timothy 3:13 in English
2 Timothy 3:13 · Berean Standard Bible
while evil men and imposters go from bad to worse, deceiving and being deceived.
Context
11mateso na taabu, yaani mambo yote yaliyonipata huko Antiokia, Ikonio na Listra, mateso yote niliyostahimili, lakini Bwana aliniokoa katika hayo yote. 12Naam, yeyote anayetaka kuishi maisha ya utauwa ndani ya Kristo Yesu atateswa. 13Lakini watu waovu na wadanganyaji watazidi kuwa waovu, wakidanganya na kudanganyika. 14Bali wewe, udumu katika yale uliyojifunza na kuyaamini kwa uthabiti, ukitambua ya kuwa ulijifunza hayo kutoka kwa nani, 15na jinsi ambavyo tangu utoto umeyajua Maandiko matakatifu, ambayo yanaweza kukuhekimisha upate wokovu kwa njia ya imani katika Kristo Yesu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.