2 Timotheo 3:12
2 Timothy 3:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Naam, yeyote anayetaka kuishi maisha ya utauwa ndani ya Kristo Yesu atateswa.
2 Timothy 3:12 in English
2 Timothy 3:12 · Berean Standard Bible
Indeed, all who desire to live godly lives in Christ Jesus will be persecuted,
Context
10Lakini wewe umeyajua mafundisho yangu, mwenendo, makusudi, imani, uvumilivu, upendo, ustahimilivu, 11mateso na taabu, yaani mambo yote yaliyonipata huko Antiokia, Ikonio na Listra, mateso yote niliyostahimili, lakini Bwana aliniokoa katika hayo yote. 12Naam, yeyote anayetaka kuishi maisha ya utauwa ndani ya Kristo Yesu atateswa. 13Lakini watu waovu na wadanganyaji watazidi kuwa waovu, wakidanganya na kudanganyika. 14Bali wewe, udumu katika yale uliyojifunza na kuyaamini kwa uthabiti, ukitambua ya kuwa ulijifunza hayo kutoka kwa nani,
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.