Native Bible

2 Timothy 2:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Vumilia taabu pamoja nasi kama askari mwema wa Kristo Yesu.

2 Timothy 2:3 in English

2 Timothy 2:3 · Berean Standard Bible

Join me in suffering, like a good soldier of Christ Jesus.

Context

1Basi, wewe mwanangu, uwe hodari katika neema iliyo ndani ya Kristo Yesu. 2Nayo mambo yale uliyonisikia nikiyasema mbele ya mashahidi wengi, uwakabidhi watu waaminifu watakaoweza kuwafundisha watu wengine vilevile. 3Vumilia taabu pamoja nasi kama askari mwema wa Kristo Yesu. 4Hakuna askari yeyote ambaye akiwa vitani hujishughulisha na mambo ya kawaida ya maisha haya kwa sababu nia yake ni kumpendeza yule aliyemwandika awe askari. 5Vivyo hivyo, yeye ashindanaye katika michezo hawezi kupewa tuzo ya ushindi asiposhindana kulingana na kanuni za mashindano.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.