2 Timotheo 2:14
2 Timothy 2:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Endelea kuwakumbusha mambo haya ukiwaonya mbele za Bwana waache kushindana kwa maneno ambayo hayana faida yoyote bali huwaangamiza tu wale wanaoyasikia.
2 Timothy 2:14 in English
2 Timothy 2:14 · Berean Standard Bible
Remind the believers of these things, charging them before God * to avoid quarreling over words, which succeeds only in leading the listeners to ruin.
Context
12Kama tukistahimili,
pia tutatawala pamoja naye.
Kama tukimkana yeye,
naye atatukana sisi. 13Kama tusipoamini,
yeye hudumu kuwa mwaminifu,
kwa maana hawezi kujikana mwenyewe. 14Endelea kuwakumbusha mambo haya ukiwaonya mbele za Bwana waache kushindana kwa maneno ambayo hayana faida yoyote bali huwaangamiza tu wale wanaoyasikia. 15Jitahidi kujionyesha kwa Mungu kuwa umekubaliwa naye, mtendakazi asiye na sababu ya kuona aibu, ukilitumia kwa usahihi neno la kweli. 16Jiepushe na maneno mabaya, yasiyo na maana, yasiyo ya utauwa, kwa maana hayo huzidi kuwatosa watu katika kukosa heshima kwa Mungu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.