2 Timotheo 1:3
2 Timothy 1:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ninamshukuru Mungu, ninayemtumikia kwa dhamiri safi, kama walivyofanya baba zangu, ninapokukumbuka usiku na mchana katika maombi yangu.
2 Timothy 1:3 in English
2 Timothy 1:3 · Berean Standard Bible
I thank God, whom I serve with a clear conscience as did my forefathers, as I constantly remember you night and day in my prayers.
Context
1Paulo mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu, kulingana na ile ahadi ya uzima uliomo ndani ya Kristo Yesu. 2Kwa Timotheo, mwanangu mpendwa:
Neema, rehema na amani itokayo kwa Mungu Baba, na kwa Kristo Yesu Bwana wetu. 3Ninamshukuru Mungu, ninayemtumikia kwa dhamiri safi, kama walivyofanya baba zangu, ninapokukumbuka usiku na mchana katika maombi yangu. 4Nikiyakumbuka machozi yako, ninatamani sana kukuona ili nipate kujawa na furaha. 5Nimekuwa nikiikumbuka imani yako ya kweli, waliokuwa nayo bibi yako Loisi na mama yako Eunike na ambayo mimi ninasadiki sasa wewe pia unayo.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.