2 Timotheo 1:11
2 Timothy 1:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nami nimewekwa kuwa mhubiri, mtume na mwalimu wa Injili hii.
2 Timothy 1:11 in English
2 Timothy 1:11 · Berean Standard Bible
to which I was appointed as a preacher, an apostle, and a teacher.
Context
9ambaye alituokoa na kutuita katika mwito mtakatifu: si kwa kadiri ya matendo yetu mema bali kwa sababu ya kusudi lake mwenyewe na neema yake. Neema hii tulipewa katika Kristo Yesu tangu milele. 10Lakini sasa imefunuliwa kwa kudhihirishwa kwake Mwokozi wetu, Kristo Yesu, ambaye amebatilisha mauti na kuleta uzima na kutokufa kwa njia ya Injili. 11Nami nimewekwa kuwa mhubiri, mtume na mwalimu wa Injili hii. 12Hii ndiyo sababu ninateseka namna hii, lakini sioni haya kwa maana ninamjua yeye niliyemwamini, na kusadiki ya kuwa anaweza kukilinda kile nilichokiweka amana kwake hadi siku ile. 13Shika kwa uthabiti kielelezo cha mafundisho yenye uzima yale uliyoyasikia kwangu, pamoja na imani na upendo katika Kristo Yesu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.