2 Wathesalonike 1:8
2 Thessalonians 1:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Atawaadhibu wale wasiomjua Mungu na ambao hawakuitii Injili ya Bwana wetu Yesu.
2 Thessalonians 1:8 in English
2 Thessalonians 1:8 · Berean Standard Bible
in blazing fire, inflicting vengeance on those who do not know God and do not obey the gospel of our Lord Jesus.
Context
6Mungu ni mwenye haki: yeye atawalipa mateso wale wawatesao ninyi 7na kuwapa ninyi mnaoteseka raha pamoja na sisi, wakati Bwana Yesu atakapodhihirishwa kutoka mbinguni katika mwali wa moto pamoja na malaika wake wenye nguvu. 8Atawaadhibu wale wasiomjua Mungu na ambao hawakuitii Injili ya Bwana wetu Yesu. 9Wataadhibiwa kwa uangamivu wa milele na kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa uweza wake, 10siku hiyo atakapokuja kutukuzwa katika watakatifu wake na kustaajabiwa miongoni mwa wote walioamini. Ninyi pia mtakuwa miongoni mwa hawa kwa sababu mliamini ushuhuda wetu kwenu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.