Native Bible

2 Samuel 6:1 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Tena Daudi akakusanya watu 30,000 wa Israeli waliochaguliwa.

2 Samuel 6:1 in English

2 Samuel 6:1 · Berean Standard Bible

David again assembled the chosen men of Israel, thirty thousand in all.

Context

1Tena Daudi akakusanya watu 30,000 wa Israeli waliochaguliwa. 2Yeye na watu wake wote wakatoka Baala ya Yuda* kulipandisha Sanduku la Mungu kutoka huko, linaloitwa kwa Jina, naam, jina la Bwana Mwenye Nguvu Zote, ambaye anaketi katika kiti cha enzi kati ya makerubi walioko juu ya hilo Sanduku. 3Wakaweka hilo Sanduku la Mungu juu ya gari jipya la kukokotwa na kulileta kutoka nyumba ya Abinadabu, iliyokuwa juu ya kilima. Uza na Ahio, wana wa Abinadabu, walikuwa wakiongoza hilo gari jipya la kukokotwa

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.