Native Bible

2 Samuel 5:22 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Wafilisti walikwea kwa mara nyingine na kusambaa katika Bonde la Warefai.

2 Samuel 5:22 in English

2 Samuel 5:22 · Berean Standard Bible

Once again the Philistines came up and spread out in the Valley of Rephaim.

Context

20Ndipo Daudi akaenda mpaka Baal-Perasimu, na huko akawashinda Wafilisti. Akasema, “Kama mafuriko yafurikavyo, Bwana amewafurikia adui zangu mbele yangu.” Kwa hiyo mahali hapo pakaitwa Baal-Perasimu.* 21Wafilisti wakaiacha miungu yao huko, naye Daudi na watu wake wakaichukua. 22Wafilisti walikwea kwa mara nyingine na kusambaa katika Bonde la Warefai. 23Kwa hiyo Daudi akamuuliza Bwana, naye akamjibu, “Usipande moja kwa moja, bali wazungukie kwa nyuma na uwashambulie mbele ya miti ya miforosadi. 24Mara utakaposikia sauti ya kutembea kutoka kwenye vilele vya miti ya miforosadi, nenda haraka, kwa sababu hiyo itamaanisha kuwa Bwana ametangulia mbele yako kupiga jeshi la Wafilisti.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.