2 Samweli 21:21
2 Samuel 21:21 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Alipowadhihaki Israeli, Yonathani mwana wa Shimea, nduguye Daudi, akamuua.
2 Samuel 21:21 in English
2 Samuel 21:21 · Berean Standard Bible
and when he taunted Israel, Jonathan the son of David’s brother Shimei * killed him.
Context
19Katika vita vingine na Wafilisti huko Gobu, Elhanani mwana wa Yaare-Oregimu, Mbethlehemu, alimuua nduguye Goliathi, Mgiti, ambaye mkuki wake ulikuwa na mpini kama mti wa mfumaji. 20Katika vita vingine tena, vilivyopiganwa huko Gathi, kulikuwako na mtu mmoja mkubwa mwenye vidole sita katika kila mkono na vidole sita kila mguu, jumla vidole ishirini na vinne. Yeye alikuwa pia mzao wa Mrefai. 21Alipowadhihaki Israeli, Yonathani mwana wa Shimea, nduguye Daudi, akamuua. 22Hawa wanne walikuwa wazao wa Warefai huko Gathi, nao walianguka kwa mikono ya Daudi na watu wake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.