Native Bible

2 Samuel 2:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Wakati huo Abneri mwana wa Neri, jemadari wa jeshi la Sauli, alikuwa amemchukua Ish-Boshethi mwana wa Sauli na kumleta hadi Mahanaimu.

2 Samuel 2:8 in English

2 Samuel 2:8 · Berean Standard Bible

Meanwhile, Abner son of Ner, the commander of Saul’s army, took Saul’s son Ish-bosheth,* moved him to Mahanaim,

Context

6Sasa Bwana na awaonyeshe wema na uaminifu, nami pia nitawaonyesha wema ule ule kwa kuwa mmefanya jambo hili. 7Sasa basi, kuweni hodari na mashujaa, kwa maana bwana wenu Sauli amekufa, nayo nyumba ya Yuda imenitia mafuta niwe mfalme juu yao.” 8Wakati huo Abneri mwana wa Neri, jemadari wa jeshi la Sauli, alikuwa amemchukua Ish-Boshethi mwana wa Sauli na kumleta hadi Mahanaimu. 9Akamweka awe mfalme juu ya nchi ya Gileadi, Waasheri,* Yezreeli, Efraimu, Benyamini na Israeli yote. 10Ish-Boshethi* mwana wa Sauli alikuwa na umri wa miaka arobaini alipoanza kutawala Israeli, naye akatawala miaka miwili. Hata hivyo, nyumba ya Yuda ikamfuata Daudi.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.