2 Samweli 2:11
2 Samuel 2:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Muda ambao Daudi alikuwa mfalme juu ya nyumba ya Yuda huko Hebroni ilikuwa miaka saba na miezi sita.
2 Samuel 2:11 in English
2 Samuel 2:11 · Berean Standard Bible
And the length of time that David was king in Hebron over the house of Judah was seven years and six months.
Context
9Akamweka awe mfalme juu ya nchi ya Gileadi, Waasheri,* Yezreeli, Efraimu, Benyamini na Israeli yote. 10Ish-Boshethi* mwana wa Sauli alikuwa na umri wa miaka arobaini alipoanza kutawala Israeli, naye akatawala miaka miwili. Hata hivyo, nyumba ya Yuda ikamfuata Daudi. 11Muda ambao Daudi alikuwa mfalme juu ya nyumba ya Yuda huko Hebroni ilikuwa miaka saba na miezi sita. 12Abneri mwana wa Neri, pamoja na watu wa Ish-Boshethi mwana wa Sauli, wakatoka Mahanaimu kwenda Gibeoni. 13Yoabu mwana wa Seruya na watu wa Daudi wakatoka na kukutana nao kwenye bwawa la Gibeoni. Kikundi kimoja kiliketi upande mmoja wa bwawa, na kikundi kingine upande wa pili.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.