Native Bible

2 Samuel 14:28 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Absalomu akaishi miaka miwili huko Yerusalemu pasipo kuuona uso wa mfalme.

2 Samuel 14:28 in English

2 Samuel 14:28 · Berean Standard Bible

Now Absalom lived in Jerusalem two years without seeing the face of the king.

Context

26Kila mara aliponyoa nywele za kichwa chake, kwa kuwa alikuwa akinyoa mara kwa mara zilipokuwa zinamwia nzito, alizipima uzito wake ulikuwa shekeli mia mbili kwa kipimo cha kifalme.* 27Walizaliwa wana watatu na binti mmoja kwa Absalomu. Jina la binti yake aliitwa Tamari, naye akawa mwanamke mzuri wa sura. 28Absalomu akaishi miaka miwili huko Yerusalemu pasipo kuuona uso wa mfalme. 29Basi Absalomu akamwita Yoabu kwa kusudi la kumtuma kwa mfalme, lakini Yoabu akakataa kuja kwa Absalomu. Ndipo akamwita tena mara ya pili, lakini pia akakataa kuja. 30Ndipo akawaambia watumishi wake, “Tazama, shamba la Yoabu liko jirani na langu, naye ana shayiri humo. Nendeni mkalitie moto.” Kisha watumishi wa Absalomu wakalitia moto shamba hilo.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.