2 Samweli 13:3
2 Samuel 13:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Basi Amnoni alikuwa na rafiki jina lake Yonadabu mwana wa Shimea,* nduguye Daudi. Yonadabu alikuwa mtu wa hila nyingi sana.
2 Samuel 13:3 in English
2 Samuel 13:3 · Berean Standard Bible
Now Amnon had a friend named Jonadab, the son of David’s brother Shimeah.* Jonadab was a very shrewd man,
Context
1Ikawa baada ya hayo, Amnoni mwana wa Daudi akampenda Tamari, umbu lake Absalomu mwana wa Daudi, ambaye alikuwa mzuri wa sura. 2Amnoni akasumbuka sana kuhusu Tamari hata akaugua, kwa kuwa Tamari alikuwa bikira, na ilionekana kwamba haiwezekani Amnoni kumfanyia jambo lolote. 3Basi Amnoni alikuwa na rafiki jina lake Yonadabu mwana wa Shimea,* nduguye Daudi. Yonadabu alikuwa mtu wa hila nyingi sana. 4Akamuuliza Amnoni, “Wewe ni mtoto wa mfalme; kwa nini siku baada ya siku unaonekana kukonda? Hutaniambia?”
Amnoni akamwambia, “Ninampenda Tamari, dada yake Absalomu ndugu yangu.” 5Yonadabu akamwambia, “Nenda ukalale kitandani na ujifanye kuwa mgonjwa. Baba yako atakapokuja kukuona mwambie, ‘Ningependa Tamari dada yangu aje kunipatia chochote ili nile. Tafadhali mruhusu aje na kuniandalia chakula mbele yangu ningali ninamwona, ili nipate kula kutoka mkononi mwake.’ ”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.