2 Samweli 11:26
2 Samuel 11:26 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mke wa Uria aliposikia kwamba mumewe amekufa, akamwombolezea.
2 Samuel 11:26 in English
2 Samuel 11:26 · Berean Standard Bible
When Uriah’s wife heard that her husband was dead, she mourned for him.
Context
24Ndipo wapiga upinde walitupa mishale kwa watumishi wako kutoka ukutani, na baadhi ya watu wa mfalme wakafa. Zaidi ya hayo, Uria, Mhiti, mtumishi wako amekufa.” 25Daudi akamwambia mjumbe, “Ukamwambie Yoabu hivi, ‘Jambo hili lisikutie wasiwasi, upanga hula huyu sawa na ulavyo mwingine. Zidisha mashambulizi dhidi ya mji na uangamize.’ Mwambie Yoabu hivi ili kumtia moyo.” 26Mke wa Uria aliposikia kwamba mumewe amekufa, akamwombolezea. 27Baada ya muda wa maombolezo kwisha, Daudi akamtaka aletwe nyumbani kwake, naye akawa mkewe, na akamzalia mwana. Lakini jambo alilokuwa amefanya Daudi lilimchukiza Bwana.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.