2 Samweli 11:16
2 Samuel 11:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hivyo Yoabu alipokuwa ameuzingira mji kwa jeshi, akamweka Uria mahali ambapo alijua kuwa ulinzi wa adui ulikuwa imara sana.
2 Samuel 11:16 in English
2 Samuel 11:16 · Berean Standard Bible
So as Joab besieged the city, he assigned Uriah to a place where he saw the strongest enemy soldiers.
Context
14Asubuhi yake Daudi akamwandikia Yoabu barua, akamtuma Uria kuipeleka. 15Ndani ya barua aliandika, “Mweke Uria mstari wa mbele mahali ambapo mapigano ni makali sana. Kisha wewe uondoke ili Uria aangushwe chini na kuuawa.” 16Hivyo Yoabu alipokuwa ameuzingira mji kwa jeshi, akamweka Uria mahali ambapo alijua kuwa ulinzi wa adui ulikuwa imara sana. 17Wakati watu wa mjini walipotoka kwenda kupigana dhidi ya Yoabu, baadhi ya watu katika jeshi la Daudi wakauawa, zaidi ya hayo, Uria, Mhiti, akafa. 18Yoabu akampelekea Daudi maelezo yote ya vita.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.