Native Bible

2 Samuel 11:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Asubuhi yake Daudi akamwandikia Yoabu barua, akamtuma Uria kuipeleka.

2 Samuel 11:14 in English

2 Samuel 11:14 · Berean Standard Bible

The next morning David wrote a letter to Joab and sent it with Uriah.

Context

12Ndipo Daudi akamwambia, “Kaa hapa siku moja zaidi, nami kesho nitakutuma urudi.” Kwa hiyo Uria akakaa Yerusalemu siku ile na siku iliyofuata. 13Kwa ukaribisho wa Daudi, Uria akala na kunywa pamoja naye, Daudi akamlevya. Lakini jioni Uria alitoka kwenda kulala juu ya mkeka wake miongoni mwa watumishi wa bwana wake, hakwenda nyumbani. 14Asubuhi yake Daudi akamwandikia Yoabu barua, akamtuma Uria kuipeleka. 15Ndani ya barua aliandika, “Mweke Uria mstari wa mbele mahali ambapo mapigano ni makali sana. Kisha wewe uondoke ili Uria aangushwe chini na kuuawa.” 16Hivyo Yoabu alipokuwa ameuzingira mji kwa jeshi, akamweka Uria mahali ambapo alijua kuwa ulinzi wa adui ulikuwa imara sana.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.