2 Samweli 1:24
2 Samuel 1:24 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Enyi binti za Israeli, lieni kwa ajili ya Sauli, ambaye aliwavika nguo nyekundu na maridadi, ambaye aliremba mavazi yenu kwa mapambo ya dhahabu.
2 Samuel 1:24 in English
2 Samuel 1:24 · Berean Standard Bible
O daughters of Israel, weep for Saul, who clothed you in scarlet and luxury, who decked your garments with ornaments of gold.
Context
22Kutokana na damu ya waliouawa,
kutokana na miili ya wenye nguvu,
ule upinde wa Yonathani haukugeuka nyuma.
Upanga wa Sauli haukurudi bure. 23“Sauli na Yonathani,
maishani walipendwa na kuneemeka,
na katika kifo hawakutengana.
Walikuwa wepesi kuliko tai,
walikuwa na nguvu kuliko simba. 24“Enyi binti za Israeli,
lieni kwa ajili ya Sauli,
ambaye aliwavika nguo
nyekundu na maridadi,
ambaye aliremba mavazi yenu
kwa mapambo ya dhahabu. 25“Tazama jinsi mashujaa
walivyoanguka vitani!
Yonathani ameuawa
mahali pako palipoinuka. 26Nahuzunika kwa ajili yako,
Yonathani ndugu yangu,
kwangu ulikuwa mpendwa sana.
Upendo wako kwangu ulikuwa wa ajabu,
wa ajabu zaidi kuliko ule wa wanawake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.