2 Wafalme 9:4
2 Kings 9:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Basi yule kijana nabii akaenda Ramoth-Gileadi.
2 Kings 9:4 in English
2 Kings 9:4 · Berean Standard Bible
So the young prophet went to Ramoth-gilead,
Context
2Ukifika huko, mtafute Yehu mwana wa Yehoshafati, mwana wa Nimshi. Enda kwake, umtenge na wenzake, na umpeleke katika chumba cha ndani. 3Kisha chukua hii chupa na umimine mafuta juu ya kichwa chake, nawe utangaze, ‘Hivi ndivyo asemavyo Bwana: Ninakutia mafuta uwe mfalme juu ya Israeli.’ Kisha ufungue mlango na ukimbie; usikawie!” 4Basi yule kijana nabii akaenda Ramoth-Gileadi. 5Wakati alipofika, akawakuta maafisa wa jeshi wameketi pamoja, akasema, “Nina ujumbe wako, ee jemadari.”
Yehu akauliza, “Kwa yupi miongoni mwetu?”
Akamjibu, “Kwako wewe, jemadari.” 6Yehu akainuka na kuingia ndani ya nyumba. Ndipo yule nabii akamimina mafuta juu ya kichwa cha Yehu na kutangaza, “Hivi ndivyo asemavyo Bwana, Mungu wa Israeli: ‘Ninakutia mafuta uwe mfalme juu ya watu wa Bwana, yaani Israeli.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.