2 Wafalme 6:26
2 Kings 6:26 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wakati mfalme wa Israeli alipokuwa anapita juu ya ukuta, mwanamke mmoja akamlilia, “Bwana wangu mfalme, nisaidie!”
2 Kings 6:26 in English
2 Kings 6:26 · Berean Standard Bible
As the king of Israel was passing by on the wall, a woman cried out to him, “Help me, my lord the king!”
Context
24Baada ya kitambo kidogo, Ben-Hadadi mfalme wa Aramu akaandaa jeshi lake lote akapanda kwenda kuihusuru Samaria. 25Kukawa na njaa kuu katika mji. Samaria ilizingirwa kwa muda mrefu, kiasi kwamba kichwa cha punda kiliuzwa kwa shekeli themanini* za fedha, na robo ya kibaba* cha mavi ya njiwa kiliuzwa kwa shekeli tano* za fedha. 26Wakati mfalme wa Israeli alipokuwa anapita juu ya ukuta, mwanamke mmoja akamlilia, “Bwana wangu mfalme, nisaidie!” 27Mfalme akajibu, “Ikiwa Bwana hakusaidii, nitakutolea wapi msaada? Je, ni kutoka kwenye sakafu ya kupuria? Au kwenye shinikizo la divai?” 28Kisha akamuuliza, “Kwani kuna nini?”
Yule mwanamke akamjibu, “Huyu mwanamke aliniambia, ‘Mtoe mwanao ili tupate kumla leo, na kesho tutamla mwanangu.’
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.