Native Bible

2 Kings 5:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Akamwambia bibi yake, “Kama bwana wangu angelimwona nabii aliyeko Samaria! Angemponya ukoma wake.”

2 Kings 5:3 in English

2 Kings 5:3 · Berean Standard Bible

She said to her mistress, “If only my master would go to the prophet who is in Samaria, he would cure him of his leprosy.”

Context

1Wakati huu, Naamani alikuwa jemadari wa jeshi la mfalme wa Aramu. Alikuwa mtu mkuu mbele ya bwana wake na aliyeheshimiwa sana, kwa sababu kupitia kwake, Bwana alikuwa amewapa Aramu ushindi. Alikuwa askari shujaa, lakini alikuwa na ukoma.* 2Siku hizo vikosi kutoka Aramu vilikuwa vimekwenda na vikawa vimemteka msichana kutoka Israeli, naye akamtumikia mkewe Naamani. 3Akamwambia bibi yake, “Kama bwana wangu angelimwona nabii aliyeko Samaria! Angemponya ukoma wake.” 4Naamani akaenda kwa bwana wake na kumwambia alichosema yule msichana kutoka Israeli. 5Mfalme wa Aramu* akamjibu, “Hakika, nenda. Nitatuma barua kwa mfalme wa Israeli.” Kwa hiyo Naamani akaondoka, akiwa amechukua talanta kumi* za fedha, shekeli 6,000 za dhahabu,* na mivao kumi ya mavazi.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.