2 Wafalme 4:21
2 Kings 4:21 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mama akampandisha na kumlaza juu ya kitanda cha yule mtu wa Mungu, kisha akafunga mlango, akatoka nje.
2 Kings 4:21 in English
2 Kings 4:21 · Berean Standard Bible
And she went up and laid him on the bed of the man of God. Then she shut the door and went out.
Context
19Akamwambia baba yake, “Kichwa changu! Kichwa changu!”
Baba yake akamwambia mtumishi, “Mchukue umpeleke kwa mama yake.” 20Baada ya mtumishi kumbeba na kumpeleka kwa mama yake, mtoto akaketi mapajani mwa mama yake mpaka adhuhuri, kisha akafa. 21Mama akampandisha na kumlaza juu ya kitanda cha yule mtu wa Mungu, kisha akafunga mlango, akatoka nje. 22Akamwita mume wake na kusema, “Tafadhali mtume mmoja miongoni mwa mtumishi pamoja na punda ili niweze kwenda kwa mtu wa Mungu haraka na kurudi.” 23Mume wake akamuuliza, “Kwa nini uende kwake leo? Leo si mwandamo wa mwezi, wala si Sabato.”
Mwanamke akasema, “Yote ni sawa.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.