Native Bible

2 Kings 3:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Lakini baada ya Ahabu kufa, mfalme wa Moabu aliasi dhidi ya mfalme wa Israeli.

2 Kings 3:5 in English

2 Kings 3:5 · Berean Standard Bible

But after the death of Ahab, the king of Moab rebelled against the king of Israel.

Context

3Hata hivyo akashikamana na dhambi za Yeroboamu mwana wa Nebati, ambazo alisababisha Israeli kuzitenda, wala hakuziacha. 4Basi Mesha mfalme wa Moabu akafuga kondoo, naye akawa ampatie mfalme wa Israeli wana-kondoo 100,000 pamoja na sufu ya kondoo dume 100,000. 5Lakini baada ya Ahabu kufa, mfalme wa Moabu aliasi dhidi ya mfalme wa Israeli. 6Kwa hiyo wakati ule Mfalme Yehoramu akaondoka kutoka Samaria na kukusanya Israeli yote tayari kwenda vitani. 7Akapeleka pia ujumbe ufuatao kwa Yehoshafati mfalme wa Yuda: “Mfalme wa Moabu ameasi dhidi yangu. Je, utakwenda pamoja nami kupigana dhidi ya Moabu?” Akajibu, “Nitakwenda pamoja nawe. Mimi ni kama wewe, watu wangu ni kama watu wako, farasi wangu ni kama farasi wako.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.