Native Bible

2 Kings 3:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Hili ni jambo rahisi machoni pa Bwana. Pia ataitia Moabu mikononi mwenu.

2 Kings 3:18 in English

2 Kings 3:18 · Berean Standard Bible

This is a simple matter in the sight of the LORD, and He will also deliver the Moabites into your hand.

Context

16naye akasema, “Hivi ndivyo asemavyo Bwana, ‘Chimbeni bonde hili lijae mahandaki.’ 17Kwa kuwa hivi ndivyo asemavyo Bwana: Hamtaona upepo wala mvua, lakini bonde hili litajaa maji, nanyi pamoja na ngʼombe wenu na wanyama wenu wengine mtakunywa. 18Hili ni jambo rahisi machoni pa Bwana. Pia ataitia Moabu mikononi mwenu. 19Mtaushinda kila mji wenye ngome na kila mji mkubwa. Mtakata kila mti ulio mzuri, mtaziba chemchemi zote, na kuharibu kila shamba zuri kwa mawe.” 20Kesho yake asubuhi, karibu na wakati wa kutoa dhabihu ya asubuhi, tazama, maji yakawa yanatiririka kutoka upande wa Edomu! Nayo nchi ikajaa maji.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.