Native Bible

2 Kings 20:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kabla Isaya hajaondoka katika ua wa kati, neno la Bwana likamjia, akaambiwa:

2 Kings 20:4 in English

2 Kings 20:4 · Berean Standard Bible

Before Isaiah had left the middle courtyard,* the word of the LORD came to him, saying,

Context

2Hezekia akaelekeza uso wake ukutani, akamwomba Bwana: 3“Ee Bwana, kumbuka jinsi nilivyoenenda mbele zako kwa uaminifu na kujitoa kwa moyo wangu wote, na kufanya yaliyo mema machoni pako.” Naye Hezekia akalia kwa uchungu. 4Kabla Isaya hajaondoka katika ua wa kati, neno la Bwana likamjia, akaambiwa: 5“Rudi ukamwambie Hezekia, kiongozi wa watu wangu, ‘Hili ndilo asemalo Bwana, Mungu wa baba yako Daudi: Nimeyasikia maombi yako na nimeona machozi yako; nitakuponya. Siku ya tatu kuanzia sasa utapanda kwenda Hekalu la Bwana. 6Nitakuongezea miaka kumi na mitano katika maisha yako. Nami nitakuokoa wewe pamoja na mji huu mkononi mwa mfalme wa Ashuru. Nitaulinda mji huu kwa ajili yangu, na kwa ajili ya mtumishi wangu Daudi!’ ”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.