2 Wafalme 18:3
2 Kings 18:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Akafanya yaliyo mema machoni pa Bwana, kama Daudi baba yake alivyofanya.
2 Kings 18:3 in English
2 Kings 18:3 · Berean Standard Bible
And he did what was right in the eyes of the LORD, just as his father David had done.
Context
1Katika mwaka wa tatu wa utawala wa Hoshea mwana wa Ela mfalme wa Israeli, Hezekia mwana wa Ahazi mfalme wa Yuda alianza kutawala. 2Alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miaka ishirini na tisa. Mama yake aliitwa Abiya binti Zekaria. 3Akafanya yaliyo mema machoni pa Bwana, kama Daudi baba yake alivyofanya. 4Akapaondoa mahali pa juu pa kuabudia miungu, akazivunja sanamu, akakatakata nguzo za Ashera. Akavunja vipande vipande ile nyoka ya shaba Mose aliyotengeneza, kwa kuwa hadi siku hizo wana wa Israeli walikuwa wanaifukizia uvumba (ilikuwa ikiitwa Nehushtani*). 5Hezekia aliweka tumaini lake kwa Bwana, Mungu wa Israeli. Hapakuwepo na mfalme mwingine wa kufanana naye miongoni mwa wafalme wa Yuda, kabla yake au baada yake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.