Native Bible

2 Kings 17:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Wakaabudu sanamu, ingawa Bwana alikuwa amesema, “Msifanye mambo haya.”

2 Kings 17:12 in English

2 Kings 17:12 · Berean Standard Bible

They served idols, although the LORD had told them, “You shall not do this thing.”*

Context

10Wakaweka mawe ya kuabudiwa na nguzo za Ashera juu ya kila kilima kirefu na chini ya kila mti uliotanda. 11Wakafukiza uvumba kila mahali palipoinuka, kama yalivyofanya yale mataifa ambayo Bwana alikuwa ameyafukuza mbele yao. Wakafanya mambo maovu ambayo yalimghadhibisha Bwana. 12Wakaabudu sanamu, ingawa Bwana alikuwa amesema, “Msifanye mambo haya.” 13Bwana akawaonya Israeli na Yuda kupitia kwa manabii na waonaji wake wote: “Acheni njia zenu mbaya. Shikeni amri na maagizo yangu, kufuatana na sheria yangu yote niliyowaagiza baba zenu kuitii ambayo niliileta kwenu kupitia kwa watumishi wangu manabii.” 14Lakini hawakusikiliza, walikuwa na shingo ngumu kama baba zao, ambao hawakumtegemea Bwana Mungu wao.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.