2 Wafalme 15:3
2 Kings 15:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Akatenda yaliyo mema machoni pa Bwana, kama Amazia baba yake alivyofanya.
2 Kings 15:3 in English
2 Kings 15:3 · Berean Standard Bible
And he did what was right in the eyes of the LORD, just as his father Amaziah had done.
Context
1Katika mwaka wa ishirini na saba wa utawala wa Yeroboamu mfalme wa Israeli, Azaria mwana wa Amazia mfalme wa Yuda alianza kutawala. 2Alikuwa na umri wa miaka kumi na sita alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miaka hamsini na miwili. Mama yake aliitwa Yekolia wa Yerusalemu. 3Akatenda yaliyo mema machoni pa Bwana, kama Amazia baba yake alivyofanya. 4Hata hivyo, mahali pa juu pa kuabudia hapakuondolewa. Watu waliendelea kutoa kafara na kufukiza uvumba huko. 5Bwana akampiga mfalme kwa ukoma mpaka siku aliyokufa, naye aliishi katika nyumba iliyotengwa peke yake. Yothamu mwana wa mfalme akawa msimamizi wa jumba la mfalme, na akawatawala watu wa nchi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.